Ayatullah Haajj Sayyid Ali Khamenei

Ayatullah Haajj Sayyid Ali Khamenei

Ayatullah Haajj Sayyid Ali Khamenei

Ayatullah Haajj Sayyid Ali Khamenei

Uongozi katika Mtazamo wa Sheria

Uongozi katika Mtazamo wa Sheria
  

Uongozi katika Mtazamo wa Sheria


http://www.leader.ir/langs/sw/index.php?p=leader_law

Uongozi katika Mtazamo wa Sheria
Vifungu vinavyozungumzia uongozi katika Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
• Ibara ya 2: Jamhuri ya Kiislamu
• Ibara ya 5: Utawala wa Faqihi muadilifu na mwenye takua
• Ibara ya 57: Vyombo vitatu vya utawala katika Jamhuri ya Kiislamu
• Ibara ya 60: Serikali
• Ibara ya 91: Baraza la Kulinda Sheria
• Ibara ya 107: Uainishaji wa Kiongozi Muadhamu unaofanywa na Baraza la Wataalamu wanaomchagua kiongozi
• Ibara ya 109: Masharti na sifa za kiongozi
• Ibara ya 110: Wajibu na mamlaka ya kiongozi
• Ibara ya 111: Kufariki dunia, kung'atuka madarakani au kuuzuliwa kiongozi
• Ibara ya 112: Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu
• Ibara ya 113: Rais wa Jamhuri
• Ibara ya 131: Kufariki dunia, kuuzuliwa au kujiuzulu Rais wa Jamhuri
• Ibara ya 142: Mali ya Kiongozi Muadhamu, Rais wa Jamhuri na viongozi wengine
• Ibara ya 157: Mkuu wa Vyombo vya Mahakama
• Ibara ya 175: Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
• Ibara ya 177: Marekebisho ya Katiba

Ibara ya Pili ya Katiba

Jamhuri ya Kiislamu ni mfumo uliosimama katika misingi ya imani ya:
1- Mwenyezi Mungu Mmoja (Lailaha Illallah). Ni yake Yeye mamlaka na sheria na ni wajibu kusalimu amri mbele yake Yeye.
2- Wahyi wa Mwenyezi Mungu na nafasi yake ya kimsingi katika kubainisha sheria.
3- Siku ya Kiyama na nafasi yake muhimu katika mwenendo wa ukamilifi wa mwanadamu kuelekea kwa Mwenyezi Mungu.
4- uadilifu wa Mwenyezi Mungu katika kuumba na kuweka sheria.
Uimamu na uongozi wa daima na mchango wake mkubwa katika kudumisha Mapinduzi ya Kiislamu.
5- Utukufu na thamani aali za mwanadamu na uhuru sambamba wajibu wake mbele ya Mwenyezi Mungu unaopatikana kupitia njia ya:
a. Ijtihadi ya kudumu ya wanazuoni wa fiqhi waliokamilisha masharti kwa mujibu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Suna za maasumu (amani ya Mwezi Mungu iwe juu yao).
b. Kutumia sayansi, fani mbalimbali na tajiriba ya maendeleo ya mwanadamu na juhudi za kuviendeleza.
c. Kupinga aina zote za dhulma na kudhuliwa, na kutawala au kutawaliwa kwa mabavu. Kuchunga uadilifu, kujitawala kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na mshikamano wa kitaifa.

Ibara ya 5

Katika kipindi cha kuwa ghaibu Imam wa zama (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake) utawala na uongozi wa umma katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utashikwa na faqihi muadilifu na mwenye takua, anayetambua masuala ya zama, shujaa na mwenye tadbiri. Mwanazuoni huyo huchukua madaraka kwa mujibu wa ibara ya 107.

Ibara ya 57

Vyombo vya utawala katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni: Bunge, Serikali na Vyombo vya Mahakama ambavyo vyote viko chini ya utawala mutlaki wa faqihi na kiongozi wa umma kwa mujibu wa ibara zinazokuja za Katiba. Kila kimoja kati ya vyombo hivyo vitatu kunajitegemea.

Ibara ya 60

Kazi za serikali, mbali na masuala ambayo kikatiba yamewekwa moja kwa moja chini ya mamlaka ya Kiongozi Muadhamu, zinatekelezwa na Rais wa Jamhuri na mawaziri.

Ibara ya 91

Ili kulinda sheria za Kiislamu na Katiba katika upande wa kutopingana maazimio ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na vitu hivyo, kutaundwa baraza litakaloitwa Baraza la Walinzi wa Katiba ambalo linajumuisha:
1- Wanazuoni sita wa fiqhi, waadilifu, wanaotambua muktadha wa zama na masuala ya wakati huo. Wanazuoni hao wanachaguliwa na Kiongozi Muadhamu.
2- Wanasheria sita wataalamu wa nyanja mbalimbali za sheria kati ya wanasheria wa Kiislamu wanaoarifishwa na Mkuu wa Vyombo vya Mahakama kwa Majlisi ya Ushari ya Kiislamu (Bunge) na kuchaguliwa kwa kura za Bunge.

Ibara ya 107

Baada ya Marja' mkuu na kiongozi adhimu wa Mapinduzi ya Kimataifa ya Kiislamu na muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ayatullahil Udhma Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ambaye alitambuliwa na kukubaliwa na karibu wananchi wote kuwa Marja' na kiongozi, uteuzi wa Kiongozi Muadhamu ni wadhifa wa Baraza la Wataalamu wanaochaguliwa na wananchi. Wataalamu hao wanachunguza na kushauriana kuhusu wanazuoni wote wa fiqhi waliokamilisha masharti yaliyotajwa kwenye ibara za 5 na 109, na kumchagua mmoja miongoni mwao ambaye atakuwa na elimu zaidi ya sheria na masuala ya kifiqhi au kisiasa na kijamii na mwenye kukubalika kwa umma, au mwenye sifa makhsusi kati ya zile zilizotajwa kwenye ibara za 109. Kinyume chake baraza la Wataalamu litamchagua na kumtangaza mmoja kati ya wanachama wake kuwa Kiongozi. Kiongozi aliyechaguliwa na Baraza la Wataalamu atachukua mamlaka ya nchi na majukumu yake yote.
Kiongozi huyo atakuwa sawa na wananchi wengine mbele ya sheria.

Ibara ya 109

Masharti na Sifa za Kiongozi
1- Uwezo wa kielimu unaohitajika kwa ajili ya kutoa fatuwa katika milango mbalimbali ya fiqhi.
2- Uadilifu na takua inayohitajika kwa ajili ya kuongoza umma wa Kiislamu.
3- Mtazamo sahihi wa kisiasa na kijamii, tadbiri, ushujaa na uwezo wa kutosha wa kuongoza.
Iwapo wenye masharti hayo watakuwa kadhaa, mtu mwenye mtazamo madhubuti zaidi wa kifiqhi na kisiasa atatangulizwa mbele ya wengine.

Ibara ya 110

Wajibu na mamlaka ya Kiongozi:
1- Kuainisha siasa kuu za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya kushauriana na Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu.
2- kusimamia utekelezaji mzuri wa siasa kuu.
3- Kuitisha kura ya maoni.
4- Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya jeshi.
5- Kutangaza vita au suluhu na kuandaa jeshi.
6- Kuteua, kuuzulu na kukubali kujiuzulu kwa:
a. Wanazuoni wa fiqhi wa Baraza la Kulinda Katiba.
b. Kiongozi mkuu wa Vyombo vya Mahakama.
c. Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
d. Mkuu wa Jeshi
e. Kamanda Mkuu wa Jeshi la Gadi ya Mapinduzi ya Kiislamu.
f. Makamanda wakuu wa vikosi vya jeshi na polisi
7- Kutatua hitilafu na kupanga uhusiano wa vyombo vitatu vikuu vya mamlaka.
8- Kutatua matatizo ya mfumo (wa Jamhuri ya Kiislamu) ambayo hayawezi kutatuliwa kwa njia za kawaida, kupitia Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu.
9- Kumpasisha Rais wa Jamhuri baada ya kuchaguliwa na wananchi. Ustahiki wa wagombea nafasi ya Urais na kuhakikisha wametimiza masharti yaliyotajwa kwenye Katiba unapaswa kupasishwa na Baraza la Kulinda Katiba kabla ya uchaguzi na kuungwa mkono na Kiongozi Muadhamu.
10- Kumuuzulu Rais wa Jamhuri kwa kuzingatia maslahi ya nchi baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu kwamba amekiuka wajibu wake wa kisheria au baada ya kura ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) ya kutokuwa na imani na Rais kwa mujibu wa ibara ya 89.
11- Kusamehe au kupunguza adhabu za watu waliopatikana na hatia katika mipaka ya sheria za Kiislamu baada ya mapendekezo ya Mkuu wa Vyombo vya Sheria.
Kiongozi Muadhamu anaweza kufawidhi baadhi ya wajibu na mamlaka yake kwa mtu mwingine.

Ibara ya 111

Wakati wowote itakapobainika kwamba Kiongozi Muadhamu hawezi kutekeleza wajibu wake za kisheria au hana mojawapo ya masharti yaliyotajwa katika ibara za 5 na 109 za Katiba, au ikaeleweka kwamba tangu awali hakuwa na baadhi ya sifa, atauzuliwa cheo hicho.
Wadhifa wa kuainisha hali hiyo ni wa Baraza la Wataalamu lililotajwa katika ibara ya 108 ya Katiba. Iwapo kiongozi atafariki dunia, kung'atuka au kuuzuliwa, wajumbe wa Baraza la Wataalamu wanawajibika kumuainisha na kumtangaza kiongozi mpya haraka iwezekanavyo. Hadi wakati wa kutangazwa kiongozi mpya, baraza linalojumuisha Rais wa Jamhuri, Mkuu wa Vyombo vya Sheria na mmoja wa wanazuoni wa fiqhi wa Baraza la Walinzi wa Katiba atakayeteuliwa na Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu, litachukua kwa muda nyadhifa zote za Kiongozi Muadhamu. Iwapo katika kipindi hicho mmoja wao atashindwa kutekeleza wajibu wake kwa sababu yoyote ile, mtu mwingine atateuliwa na Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu kwa kura nyingi za wanazuoni wa fiqhi kuchukua nafasi yake.
Baraza hilo (linalojumuisha Rais, Mkuu wa Vyombo vya Sheria na mwanazuoni wa fiqhi) litakuwa na mamlaka ya kutekeleza vifungu vya 1, 3, 5 na 10 na sehemu za (d), (e) na (f) kifungu cha 6 ibara ya 110 baada ya kupasishwa na robo tatu ya wanachama wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu.
Wakati wowote Kiongozi Muadhamu anaposhindwa kutekeleza kwa muda nyadhifa zake kutokana na maradhi au tukio jingine, baraza lililotajwa katika ibara hii litatekeleza nyadhifa zake.

Ibara ya 112

Kikao cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu kitaitishwa kwa amri ya Kiongozi Muadhamu kwa ajili ya kuainisha maslahi na kushauriana kuhusu masuala yatakayowasilishwa kwa halmashauri hiyo na kiongozi na mambo mengine yaliyotajwa kwenye katiba, wakati maazimio ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) yatakapotambuliwa na Baraza la Kulinda Katiba kuwa ni kinyume cha sheria za dini au Katiba, na bunge likakataa kutekeleza maoni ya Baraza la kulinda Katiba kwa kutilia maanani maslahi ya mfumo.
Wanachama wa kudumu na wasiokuwa wa kudumu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wanaainishwa na Kiongozi Muadhamu.
Maamuzi ya halmashauri hiyo yanatayarishwa na kupasishwa na wanachama wake na kupitishwa na Kiongozi Muadhamu.

Ibara ya 113

Baada ya Kiongozi Muadhamu, Rais wa Jamhuri ndiye kiongozi rasmi wa juu kabisa wa nchi na anawajibika kutekeleza katiba na kuongoza serikali isipokuwa katika masuala yanayofungamana moja kwa moja na Kiongozi Muadhamu.

Ibara ya 131

Iwapo Rais wa Jamhuri atafariki dunia, kuuzuliwa, kujiuzulu, kutoweka au kuumwa kwa kupindi cha zaidi ya miezi miwili, au kipindi cha uongozi wake kumalizika na Rais mpya akawa hajachaguliwa kutokana na vizuizi mbalimbali na masuala mengine kama hayo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri atachuku nyadhina na mamlaka yake kwa kuidhinishwa na Kiongozi Muadhamu. Vilevile baraza linalojumuisha Spika wa Bunge, Mkuu wa Vyombo vya Sheria na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri linawajibika kupanga taratibu za kuchaguliwa Rais mpya wa Jamhuri katika kipindi kisichozidi siku hamsini.
Iwapo Makamu wa Kwanza wa Rais atafariki dunia au kukajitokeza mambo mengine yanayomzuia kutekeleza nyadhifa zake, na kama Rais wa Jamhuri hakuwa na Makamu wa Kwanza, Kiongozi Muadhamu atamteuwa mtu mwingine kuchukua nafasi yake.

Ibara ya 142

Mali za Kiongozi Muadhamu, Rais wa Jamhuri, Makamu wa Rais wa Jamhuri, Mawaziri, wake na watoto wao zitachunguzwa na Mkuu wa Vyombo vya Sheria kabla na baada ya kuhudumu ili zisiwe zimeongezeka kinyume na njia za haki.

Ibara ya 157

Kiongozi Muadhamu anamteuwa mtu mujtahid (mtaalamu wa fiqhi na sheria za Kiislamu), muadilifu, mjuzi wa masuala ya sheria na mudiri mwenye tadbiri kutekeleza kazi za Vyombo vya Sheria kwa kipindi cha miaka mitano katika masuala yote ya kisheria, kiidara na kiutekelezaji. Mkuu wa Vyombo vya Sheria ndiye kiongozi wa juu kabisa wa vyombo vya sheria.

Ibara ya 175

Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran linapaswa kudhamini uhuru wa kusema na kueneza fikra kwa kuchunga sheria za Kiislamu na maslahi ya nchi. Kiongozi Muadhamu ndiye mwenye mamlaka ya kumteua na kumuuzulu Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu. Vilevile baraza linalowajumuisha wawakilishi wa Rais wa Jamhuri, Mkuu wa Vyombo vya Sheria na Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (wawili wa kila mmoja wao), litasimamia utendaji wa shirika hilo.
Sera na taratibu za kuendesha shirika hilo na usimamizi wa shughuli zake zinaainishwa na sheria.

Ibara ya 177

Marekebisho katika Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakati inapokuwa dharura yanafanyika kwa utaratibu ufuatao:
Baada ya Kiongozi Muadhamu kushauriana na Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu, hutuma hukumu kwa Rais wa Jamhuri akipendekeza vipengee vya kurekebishwa au kukamilishwa vya Katiba kwa Baraza la Marekebisho ya Katiba linaloundwa na wanachama wafuatao:
1- Wanachama wa Baraza la Kulinda Katiba.
2- Wakuu wa vyombo vikuu vutatu vya mamlaka
3- Wanachama wa kudumu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu
4- Wanachama watano wa Baraza la Wataalamu wa Kumchagua Kiongozi Muadhamu.
5- Watu kumi watakaochaguliwa na Kiongozi Muadhamu.
6- Wawaklishi watatu wa baraza la mawaziri
7- Wawakilishi watatu wa Vyombo vya Sheria.
8- Wawakilishi kumi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu.
9- Wawakilishi watatu wa vyuo vikuu.
Njia za kazi, jinsi ya kuchagua na masharti yake yanaainishwa na sheria.
Maazimio ya baraza hilo yanapaswa kupigiwa kura ya maoni ya taifa na kupasishwa kwa wingi mutlaki wa washiriki katika kura hiyo baada ya kupitishwa na kutiwa saini na Kiongozi Muadhamu.
http://www.leader.ir/langs/sw/index.php?p=leader_law